El Clasico: Barcelona na Madrid wakabana koo katika mechi ya kusisimua

el-clasico-
el-clasico-
Mahasidi Barcelona na Real Madrid walitoka sare tasa katika mechi ya kukata na shoka ya El Clasico ugani Nou Camp, jana usiku huku goli la Gareth Bale wa Madrid likikataliwa kwani alikua amepotea katika kipindi cha pili.

Kulingana na matokeo hayo Mabingwa Barca watasalia kileleni mwa La Liga na alama 36 sawia na Madrid ambao wamefunga magoli chache. Hii ilikua mara ya kwanza pande hizo mbiil zimetoka sare tasa kwa miaka 17.

Manchester City itapambana na mahasidi Manchester United katika nusu fainali ya  kombe la carabao, baada ya pande zote mbili kufuzu jana.

City iliilinyuka timu ya daraja la kwanza Oxford United 3-1 huku Raheem Sterling akifunga magoli mawili, nao United waliwanyuka timu ya daraja ya pili Colchester United 3-0.

Anthony Marcial na Marcus Rashford wakifunga magoli hayo kabla ya Ryan Jackson kujifunga mwenyewe. Leicester City ambao waliwanyuka Everton 4-2 kupitia penalti baada ya sare ya 2-2 , watapambana na Aston Villa ambao waliwalaza Liverpool 5-0 siku ya Jumanne.

Mchezaji wa akiba Roberto Firmino alifungia Liverpool goli la dakika ya 91 dhidi ya Monterrey na kuisadia klabu yake kufuzu kwa fainali ya kombe la klabu bingwa duniani, mjini Doha Qatar kwa ushindi wa 2-1.

Vijana  wa Mexico walikua wameswazisha kupitia Rogelio Mori katika kipindi cha kwanza baada ya Naby Keita kufungia the Reds goli la ufunguzi. Liverpool sasa watapambana na Flamengo  ya Brazil ambao walilaza Al Hilal ya  Saudi Arabia's mabao 3-1 katika fainali ya Jumamosi.

Nchini Italia Juventus walirejea kileleni mwa ligi ya  serie A kutokana na ushindi wa 2-1 dhidi ya  Sampdoria huku Paulo Dybala na  Cristiano Ronaldo wakifungaia Juve magoil yao katika kipindi cha kwanza.

Mlinda lango mkongwe Gianluigi Buffon  mwenye umri wa miaka 41 alifikia rekodi ya  Paolo Maldini ya kucheza mechi  mia sita arubaini na saba  Serie A. Juve sasa wana alama 42 tatu mbele ya Inter Milan wanaoshikilia nafasi ya pili wakiwa na mechi moja mkononi.