Elijah Manang'oi hatotetea taji lake baada ya kupata jeraha

Elijah Manang'oi anasema hatotetea taji lake ubingwa wa dunia katika mbio za mita elfu 1,500. Manang’oi mwenye umri wa miaka 26 anasema jeraha la mguu alilolipata wakati wa mazoezi limemweka nje ya mashindano hayo yatakayoandaliwa kuanzia tareha 27 mwezi huu hadi Oktoba tarehe 6.

Walio katika kikosi hicho ni pamoja na bingwa wa dunia wa chini ya miaka 20 George Manang'oi, ambaye ni nduguye, mshindi wa  medali ya fedha katika mbio za dunia na jumuiya ya madola Timothy Cheruiyot na mshindi wa shaba katika mbio za Afrika mwaka wa 2014 Ronald Kwemoi.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Manang'oi alisema,

Sad that I am not able to defend my 1500m title in Doha WC due to an ankle injury I picked in training I had no choice, it's not my fault. But GOD knows the reason why. All my Fans in the World, to Continue to have faith in me. All the best to my team mates, World silver medalist Timothy cheryiot and My younger brother World junior champion George Manangoi and Ronald Kwemoi bring it back home guys. and all competitors and event organisers.Make Doha a fun filled and successful event.

See you next season. 

GOD Bless you all.

Hayo yakijiri, kocha wa Gor Mahia Steven Pollack anaamini licha ya kunyukwa na USM Algier mabao 4-1 katika mkondo wa kwanza wa mchuano wa CAF confederations, bado wana uwezo wa kurejea kwa ushindi na kufuzu kwa awamu ya makundi.

K’Ogallo wanahitaji kuwalaza mabingwa hao wa Algeria 3-0 ugani Kasarani tarehe 29, ili kufuzu. Gor walipoteza katika awamu hio hio msimu uliopita na walinuia kupiga hatua mwaka huu. KO’gallo wanaregea nchini leo.