Owalo

Eliud Owalo ajiunga na kambi ya DP Ruto kabla ya kipute cha 2022

Aliyekuwa  mwanachama wa ANC  Eliyd Owalo  amejiunga na kambi ya naibu wa rais William Ruto kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Owalo alijizulu kama mwanachama wa ANC  cha Musalia Mudavadi  baada ya kusema kulikuwa na haja kwake kuondoka ili kutoa nafasi ndani ya chama hicho .

Kupitia taarifa siku ya jumatatu Owalo amesema Kenya inahitaji kiongozi thabiti mwenye historia ya uongozi wa kuwahusisha wote  na anayewajali watu .

Amesema baada ya kutafakari hali na  wagombeaji wa urais mwaka wa 2022 amefanya uamuzi wa  kujiunga na kundi la ‘Hustler’ .

” Pia nitamaliza safari a Bill Ruto mwaka wa 2022’ amesema kupitia taarifa yake.

Ruto: Nitaendelea kuwapigania mahustler,DP asema akiwa Kisii

Owalo  pia amesema kwamba hajaona sababu ya katiba kurekebishwa . Ameshangaa  haraka iliyopo kuifanyia katiba mageuzi  kwani hapana haja au cha msingi kinachohitaji kushughulikiwa kwa dharura .

” kwa maoni yangu tatizo letu sio katiba bali kukosa kuitekeleza katiba kikamilifu  na kutumikia matakwa na azma za wananchi’ amesema Owalo katika taarifa yake hiyo .

” Jambo la kuzua wasi wasi ni kwamba kuna kundi ambalo linalenga kuwarundika wakenya katika makundi ya  makabila yao kwa lengo la kushinda maamlaka’ ameongeza Owalo .

Umaskini sio jambo la kujivunia, Mudavadi apuuzilia mbali ‘hustler’

Owalo  amesema ili kuiokoa Kenya kutoka mgogoro wa sasa wa kiuchumi  na utata wa kisiasa  wakenya wanafaa kuungana kwa pamoja  kutafuta dhamira ya kuwaunganisha bila kujali  makabila yao  bali kwa maslahi ya taifa zima

 

 

 

 

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments