Eliud Owalo akihama chama cha Mudavadi cha ANC

Owalo
Owalo
Eliud Owalo  amejiuzulu kama mwanachama wa ANC  ,chama kinachoongozwa na Musalia Muadavdi

Katika taarifa siku ya ijumaa ,Owalo amesema  ‘muda ulifika kwake kuacha nafasi katika chama hicho’

"...  Kukiwezesha ANC kujitayarisha vilivyo na kw amazngira yafaayo kuendelea mbele bila kujibana kutokana na msimamo na maoni yake’

Pia amesema ameichukua hatua hiyo ili  kuunda nafasi ya kuzidi kuwepo urafiki wake binafsi na kiongozi wa chama hicho Musalia Mudavadi  na uhusiano wao kitaaluma na mzuri ambao umekuwepo kwa miaka zaidi ya 25.

Kujiondoa kwa Owalo kunajiri siku moja tu baada ya  Barrack Muluka pia kujizulu kama katibu mkuu wa chama hicho ili kukiwezesha kuwa na mwanzo mpya kablka ya uchaguzi mkuu wa 2022 .

Muluka  alisema kujiuzulu kwake kutampa  Mudavadi  Fursa ya  kujifanyia maamuzi yake ya kisiasa  kabla ya uchaguzi wa 2022.