Endelea tu kuwa na umama, nitaweka video yetu mitandaoni tukishiriki ngono ndio ufunge domo-Alikiba matatani

Divatheebawse-2
Divatheebawse-2
NA NICKSON TOSI

Kwa sasa Alikiba anatamba kwa wimbo wake mpya wa Dodo akimshirikisha mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobetto, wimbo ambao umemwezesha kupata ufwatilizi wa watu takriban milioni 2.3 katika mitandao ya kijamii.

Lakini kinachomuumiza maini kwa sasa msanii Alikiba ni kuwa mwanasosholaiti kwa jina  Diva the Bawse ambaye alikuwa anachumbiana naye kwa muda, ametishia kutoa kanda za video za ngono baina ya Alikiba na yeye kwa kile amesema ni kutokana na hatua ya msanii huyo kuendelea kumchafulia jina.

Alikiba amchokoza Diamond kwa kufichua anavyompenda ‘baby mama’ wake Hamisa katika video mpya

Diva amefichua kuwa mke wa Alikiba kutokea Kenya alifunganya na kutoka kwa makazi yao baada ya kufahamu kuwa mumewe Alikiba alikuwa na uhusiano na yeye.

Ameongeza kuwa aliamua kusitisha uhusiano wake na Alikiba kutokana na tabia ya msanii huyo ya kupenda wanawake wengi.

Huu hapa ni ujumbe alioandika Diva katika mtandao wake, japo kuna baadhi ya maneno yametoholewa katika lugha ya kiingereza.

Tutaendelea officialalikiba since umetuma watu weee umefanya everything behind, so many since I walked away... Trying to clean up yo image, I have videos, not just messages .. tena za chumban kwako Tabata … just because wewe ni mwanaume unafanya muziki you have no right to do what you doin cause I end up things with you, call me kigagula call me whatever .. Aliandika Diva

Alifichua kuwa yuko na miaka 31 kando na matusi aliyokuwa anapata kutoka kwa kambi ya Alikiba eti yeye ni mama wa umri mkubwa kuliko msanii huyo.

Btw I’m only 31 kwa cheti changu og cha kuzaliwa, ukiniongelea anything napost video zako thats a Promise na Picha Zako thats another hit … so we both lose respect in the society, I had nuff of kuchafuana ovyo na najua unawatuma i have evidence too, at this point i don’t care at all, truth to truth , wanaume mnahisi mwanamke ni mtu ambae utamfanyia everything everyday im not yo puppet … awe mjinga nope.Aliandika Diva

Baada ya kuchumbiana na Alikiba kwa muda, inadaiwa kuwa Diva alimfungisha virago na kumshauri arejee kwa mkewe Amina. Maajabu haya!