More enemies than Friends! Mulamwah atia nanga kwenye sanaa ya Ucheshi baada ya kutukanwa na wakenya mitandaoni

NA NICKSON TOSI

Muigizaji na mcheshi aliyebarikiwa talanta ya kuigiza na Rabana Mulamwah amelazimika kuzika ndoto yake ya kuigiza katika kaburi la sahau baada ya kuingiliwa na hata kutukanwa na baadhi ya wakenya kwenye mitandao ya kijamii.

Mulamwah ambaye alitazamiwa na wengi kutia fora katika sanaa hiyo, ameweka picha mitandaoni ikimwonyesha akichoma vazi ambalo lilikuwa kama kitambulisho chake jukwaani na hata kuonekana akitokwa na machozi katika video hiyo.

 Tazama video yenyewe hapa.

 Baada ya kuitundika video hiyo, mcheshi huyo alifuatisha ujumbe uliokuwa wa masikitiko na kuelezea machungu ambayo ameyapitia tangu kuingiliwa kwenye mitandao na watu ambao kwake alidhani ya kwamba watafanikisha ukuaji wa talanta yake.
Haikuwa rahisi kuafikia uamuzi huu ambao nimeuchukua. Poleni wenzangu, nilichodhani ya kwamba kitanifanya kuwa na furaha sasa kimegeuza maisha yangu na kuwa ya huzuni. Maadui wengi kuliko marafiki. Dhana potovu kila mara na matusi yasiyoisha. Sikuamua kufanya niliyokuwa nikifanya kwa kupata umaarufu bali kujifurahisha tu. Asanteni sana kwa mchango wenu haswa mashabiki na wengine wengi waliofanikisha kazi yangu na kwa wale walionitakia mabaya kwangu natumai sasa mmefurahia. Jukwaa ni lenu sasa na maombi yangu ni kuwa hakuna mtu yeyote ambaye atapitia yale nimepitia tena. Aliandika Mulamwah

Ufuatao ni ujumbe mwingine alioutuma mcheshi Mulamwah kwenye mtandao wake wa Twitter

Mashabiki wake walikuwa na haya ya kusema kuhusiuana na hatua ya Mulamwah

djshiti_comedian huweziiiii... Hata ukifanya nini hawatakupenda… sisi tuko mpaka na members of the family wenye tunasaidia na school fees na rent, Marafiki wenye tulileta Nairobi wengine tunazunguka nao tukifikiri niwatu but bado wanasema tutaisha coz hawaonangi kenye tunafanya ya maana na usanii😂😂😂😂😂😂😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃 wacha ujinga nunua nguo ingine kuja tufanye Comedy Nairobi city…… The Best way to Enjoy life in this Industry is to focus so much on positivity….. #Mulamwa The King of Vines… kenye hao maadui hawajui is that you are one of the most supportive Comedian… Son kama Mwenyezi MUNGU Hajakudharau Mwanadamu ninaniiiiiiii???????

abelmutua Jomba! Kesho piga rest, kesho kutwa Shati ingine ikuom alafu Thursday turudi kazi haraka faster.Wewe ni Champ buda!! Tumekutambua

djmokenya DONT GIVE UP !!!!! DONT GIVE UP KAKA

dj2one2 Mti wenye matunda ndio unaorushiwa mawe –

teamd2d  wengine wakwende