Epuka vurugu, Raila awahimiza wajumbe wa ODM katika kaunti ya Nairobi

baba
baba
Kinara wa ODM Raila Odinga amewahimiza wajumbe wa kaunti ya Nairobi kutoka chama hicho kuwa na nidhamu na umoja katika masuala ya bunge.

Raila aliwashauri wajumbe hao kuepuka vurugu wakati wa kutatua masuala mbalimbali.

Raila alizungumza maneno hayo siku ya jumanne katika mkutano uliohudhuriwa na wajumbe kutoka chama hicho.

 Raila alimhimiza kiongozi wa wachache katika bunge la Nairobi David Mberia kuhakikisha kuwa kuna usawa katika uwakilishi ndani ya kamati mbalimbali miongoni mwa wajumbe hao ili kuepuka visa vya migogoro.

Raila alisema kuwa wajumbe hao wanapaswa kutekeleza majukumu yao ili kuhakikisha kuwa wanainchi wanapata huduma wanayostahili.

Katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna aliwataka wajumbe hao kufanya kazi kwa pamoja .

Mwenyekiti wa ODM katika kaunti ya Nairobi George Aladwa alisisitiza kwamba wanachama wanastahili kuwa waaminifu kwa minajili ya kuchangia ukuaji wa chama.

Kiongozi wa wachache David Mberia alisema kuwa atahakikisha kuwa kuna usawa, uwazi, na umoja miongoni mwa wanachama.