Eriksen akaribia kujiunga na Ashley Young, Inter Milan ya Italia

inter milan
inter milan
Manchester United wamekubaliana kitita cha pauni milioni 1.2 na Inter Milan kwa mshambulizi Ashley Young. Mchezaji huyo mwenye umri wa maiaka 34 awali aliiambia United akwamba alitaka kujiunga na Inter na hajachezea klabu hio mechi tatu zilizopita.

Inaaminika kwamba ada hio inajumuisha ada ya nyongeza ambayo itatolewa iwapo Inter watashaninda Serie A msimu huu. Ikiwa uhamisho huo wa Januari utakamilika basi utatamatisha kipindi cha Young cha miaka nane na nusu Old Trafford.

Aston Villa wanatumai kutamatisha mkataba wa pauni milioni 10 kwa mshambulizi wa Genk Mbwana Samatta meneja Dean Smith akiendelea kupiga jeki safu yake ya ushambulizi. Smith anahitaji kuipa nguvu safu hii baada ya kumpoteza kiungo wa Brazil Wesley kwa muda wa msimu uliosalia kutokana na jeraha la goti alilolipata Burnley. Samatta, aliyefunga dhidi ya Liverpool katika awamu ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa msimuu huu analengwa na Villa lakini bado mkataba haujaafikiwa.

Klabu ya Inter Milan imeafikiana makubaliano binafsi na kiungo wa Denmark Christian Eriksen mwenye umri wa maiaka 27, ili wamsajili moja kwa moja lakini klabu yake ya Tottenham inaitaka Milan kuongeza dau lao mpaka Euro milioni 10. Wakati huo huo Tottenham wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji kutoka Cape Verde Ze Luis mwenye umri wa miaka 28, anayechezea klabu ya Porto.

Timu ya Kenya ya mpira wa vikapu kwa wanaume jana ilipata ushindi wake wa tatu mfululizo katika michuano ya FIBA Afro kwa ushindi wa 102-77 dhidi ya Somalia.

Eric Mutoro alikuwa nyota wa mechi hio kwa kufunga alama 31 na kupelekea ushindi wao mkubwa. Timu hiyo leo itapambana Sudan Kusini katika uwanja huo huo.

PSG imeitaka Atletico Madrid kupandisha dau lao la usajili ili kumnasa nyota wa Uruguay Edinson Cavani kutoka Euro mioni 10 mpaka 30. Mshambuliaji huyo anamaliza mkataba wake na PSG mwishoni mwa msimu huu.

Kwingineko Arsenal wanapanga kutoa pauni milioni sita ili kumnasa beki wa kushoto wa PSG Mfaransa Layvin Kurzawa wa miaka 27, kabla ya mchezaji huyo kumaliza mkataba wake na PSG mwishoni mwa msimu.