Esther Arunga kuhukumiwa leo dhidi ya kifo cha mwanawe

65852390_149009822833657_7901315362000186044_n
65852390_149009822833657_7901315362000186044_n
Esther Arunga aliyekuwa mwanahabari wa zamani hapa Kenya, atajua hatima yake leo baada ya kukiri kuwa aliwadanganya wanapolisi wa Australia kuhusu kilicho sababisha kifo cha mtoto wake.

Siku ya Jumatatu Arunga, aliiambia mahakama na kukiri kuwa alisema uongo kuhusu kilicho sababisha kifo cha mtoto wake ili kulinda mumewe, Quincy Timberlake.

Timberlake anashutumiwa kwa kuua mwana wake mwenye umri wa miaka mitatu aliyejulikana kama Sinclair.

Inasemekana kuwa Arunga alipigia huduma za dharura na kuwaambia kuwa Sinclair ameanguka chini kutoka ngazini. Hata hivyo ripoti za autopsy zilifunua kuwa Sinclair alikufa kutokana na kugongwa au kupigwa na majeraha yake yalikuwa kinyume na kuanguka.

Haikuwa mpaka Timberlake, mumewe Arunga alizuiliwa katika hospitali ya walemavu wa akili, ndipo Arunga alibadili kauli yake. Aliiambia wanapolisi kwamba alipoenda bafuni usiku wa Juni 17, 2014 alipata Quincy akimpiga Sinclair tumboni kabla ya kumgongesha kwa ukuta.

Boyle alisema kuwa Arunga alichelewesha uchunguzi dhidi ya kesi iliyomkumba mumewe kwa kutoa akaunti amabayo haikuwa sahihi. Mwanasheria wa Arunga, Katarina Prskalo, alisema aliamini kuwa Arunga alikuwa mlemavu wa kiakili.

Soma mengi