uingereza

Euro 2020: Uingereza yazimwa, Ureno yaicharaza Luxembourg

Uingereza walipoteza mechi yao ya kwanza ya kufuzu kwa Euro mwaka 2020 katika kipindi cha muongo mmoja wakati Jamuhuri ya Czech walipotoka nyuma na kushinda 2-1.

Jakub Brabec alisawazisha bap la Harry Kane la ufunguzi katika dakika ya tisa kabla ya Zdenek Ondrasek kufunga bao la ushindi katika dakika ya 85.

Kwingineko Ufaransa walisalia wa pili katika kundi H baada ya kuwanyuka Icelanda bao 1-0 huku Chile wakisalia kileleni baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Albania. Kwingineko Ureno waliwacharaza Luxembourg 3-0 huku Bernardo Silva, Cristiano Ronaldo, na Gonçalo Guedes wakifunga.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amejizolea taji la ligi ya Primia la meneja wa mwezi Septemba, baada ya matokeo mazuri. Liverpool waliwacharaza Newcastle, Chelsea na Sheffield, wakifunga mabao sita na kufungwa mawili tu kwa mechi nane walizoibuka washindi.

Paul Pogba atakosa mechi ya jumapili ijayo dhidi ya Liverpool, huku madaktari wa Manchester United wakihofia kuwa huenda akasalia nje hadi mwishoni mwa mwezi October.

The Reds ndio timu pekee yenye rekodi ya ushindi wa asilimia 100 katika jedwali na kumfanya Klopp kushinda tuzo hilo kwa miezi miwili mtawalia. Klopp sasa ameshinda tuzo hilo mara tano kwa jumla.

Kiungo huyo wa kati raia wa Ufaransa yuko Dubai kumaliza matibabu yake katika mazingira ya joto, akitumai kupona jeraha la mguu. Madaktari wa United wataamu atakaporegea wiki ijayo.

Mradi wa Nike Oregon umefungwa baada ya kocha mkuu Alberto Salazar kupigwa marufuku ya miaka minne baada ya kupatikana na makosa ya kukiuka kanuni za kutumia dawa za kusisimua misuli.

Afisa mkuu wa Nike Mark Parker amesema hatua hiyo itawasambaratisha wanacmichezo wa mradi huo. Kupigwa marufuku kwa Salazar kunafuatia uchunguzi wa miaka minne na taasisi ya kupambana na matumizi ya dawa hizo ya Marekani na kesi ya miaka miwili mahakamani.

Coco Gauff amefuzu kwa nusu fainali ya mechi za WTA Tour kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya Linz Open. Mchezaji tenis huyo wa umri wa miaka 15 raia wa Marekani alimpiku Kiki Bertens, wa Uholanzi seti za 7-6 (7-1) 6-4 huko Austria kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya mchezaji aliye kwenye orodha ya wachezji kumi bora. Atapambana na Andrea Petkovic wa Uholanzi katika nusu fainali ya leo.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments