Habari njema ndio hizi hapa jinsi ya kutembea na kutalii maeneo uyapendayo katika bageti yako ama kama huna pesa ya kutosha.
1.Pika chakula kutoka nyumbani
Si wote ambao wanaweza nunua chakula cha hotelini ama nje, kama unapesa na unaweza nunua chakula hicho pesa hizo unaweza tumia kwa kitu kingine.
Pika chakula kutoka nyumbani ili kikuwezeshe katka utalii na kutembea kwako.
2.Tembea msimu ambao si wa utalii
Kila mmoja anafahamu kuwa msimu wa utalii viru na hata nauli ama kukomboa gari hupanda bei huku ikiwafanya wengi kutmia pesa nyingi katika utalii wao
Msimu ambao si wa utalii bidhaa na nauli huwa katika bei nafuu.
3.Ishi na kama wananchi wa kawaida
Endapo utafaulu kuenda kutalii maeneo tofauti nchini usiishi kama mtalii bali ishi kama wananchi wa eneo hilo ili husiuziwe vitu kwa bei ghali mno
Watu wengi huuza bidhaa kwa bei ghali endapo watakuona wewe ni mtalii wa eneo hilo.
4.Jua muda wa kutalii
Si wote ambao wanajua muda mwema wa kutalii au kupanga jambo fulani, endapo utachagua muda wako vibaya haya basi utalii wakona muda wako utakuwa umekwisha bure na kuharibu pesa zako.
5.Tembea na vikundi
Vikundi upunguza gharama ya kutalii kwa maana watu wengi hugawana gharama tofauti na kisha kufanikisha utalii wako.