Fahamu kilichomfanya Massawe kuzima kipaza sauti katika mahojiano na Lucy

Massawe Jappani amelazimika kuzima kipaza sauti na kucheza muziki baada ya Lucy kuangua kilio akisimulia mahangaiko aliyoyapata kutoka kwa mumewe Ken.

Katika mahojiano yaliyochukuwa saa moja, Lucy amefunguka mwanzo mwisho kero la bwanake.

Wanandoa hawa wamejaliwa mtoto mmoja.

https://www.instagram.com/p/B5C_h66Agpl/

Ndoa yao ilisheheni vita na kisirani kama alivyosimulia Lucy,

"Nilitoka kazini kama nimechelewa. Hapo akaanza kunifokea na kuniuliza kwa nini nimechelewa..." Alianza kusimulia.

"Ghafla akaanza kuninyeshea mangumi, mateke na kutishia kuniua. Alisema ataniua mtoto wetu abaki bila mama..."

"Alikuwa ameiwasha sauti ya redio juu zaidi ili majirani wasiweze kuskia..."

Kitu na ambacho hakukielewa kabla aolewe na Ken ni kwamba alikuwa mwizi.

Ila je? Mbona Lucy azidi kuvumia katika ndoa dhalimu?

"Nilipimwa nikapatikana na virusi vya UKIMWI. Nikashangaa nijiuwe ama nifanye nini. Kumbe yeye ndiye aliniambukiza na akawa anakunywa kisirisiri kama sijui. Kwa hivyo nikasema tu tuishi kwa sababu kumpata mtu mwingine haingekuwa rahisi..."

Hadithi iliyosimuliwa na binti huyu imemfanya abubujikwe na machozi huku akiangua kilio kupelekea kipaza sauti kuzimwa ili atulie.

Baadaye Massawe aliendelea na mahojiano hayo.