Fahamu kwa nini Sonko alilazimika kukatiza malalamishi yake kwa Uhuru

Sonko
Sonko
Gavana wa Nairobi Mike Sonko hapo jana alilazimika kukatiza hotuba yake katika Bomas kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti ya BBI, baada ya kutoa malalamishi yake kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Sonko, ambaye alikuwa amealikwa jukwaani na mwenyekiti wa baraza la magavana na ambaye pia ni gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya, alisema kuhusu mjane anayenyanyaswa na walaghai.

"Kuna widow ambaye bwana yake alikuwa chef ya baba yako.. tunaomba proposal yetu... kwa zile proposals tuweze ku deal na cartels..." Sonko alisema.

Lakini alipokuwa akisema haya, wajumbe wakaanza kuimba BBI...BBI...na kulazimu Sonko kukatisha ujumbe wake.

"Hataa hii mambo naongelelea ni BBI. Jana wakati hii ripoti ilitolewa nilifurahi kwa sababau uliongelelea joblessness ..." aliongeza.

Aidha Sonko alisema kuwa wasimamizi wa hafla hiyo hawakuwajibika ipasavyo.

"...organiser wameanguka wote vile watu wanakaribishwa hapa ni mbovu... rais umekuwa ukinitetea sana nikidhulumiwa, " alisema.

Kwa sasa kenya inatazamia kuwa na Waziri Mkuu kulingana na mapendekezo ya BBI na iwapo yatatekelezwa.