unnamed

Faini aliyopewa Inspekta Mwala ni nyepesi mno, familia ya Ismael yateta

Ndugu wa ukoo wa Ismael Mangi aliyegongwa na kuuawa papo kwa hapo na muigizaji wa runinga Inspekta Mwala sasa yalalama.

Davis Mwabili almaarufu kama Inspekta Mwala alihusika katika ajali Agosti 26  na kugonga Ismael, 36 katika barabara kuu ya Kaloleni- Mazeras.

Taarifa za polisi zilionyesha kuwa Mwala alikuwa anasafiri kutoka hafla ya mazishi kuelekea Mombasa alipohusika katika ajali hii.

Soma hadithi nyingine:

Mali ya SDA Ibara yaporwa, Divai takatifu na mkate wa ekaristi havipo

 Maafisa wa polisi walifika ghafla kumkinga na wananchi waliotaka kumvuruga baada ya kisa hicho.

Jamaa na ndugu sasa wanahoji kuwa kiwango cha faini aliyopewa na mahakama ni nyepesi mno.

Mahakama ya Mombasa ilimtoza faini ya 30,000 pesa taslimu kwa kusababisha kifo au kifungo cha mwaka mmoja jela.

Soma hadithi nyingine:

 

(+Picha) : Konde Boy achapisha picha na mamake, wanafanana sana

Ndugu zake sasa wanahoji kuwa faini ya 30,000 ni kiwango cha chini sana ukilinganisha na 40,000 alizotoa kama dhamana punde tu baada ya kumgonga Mangi.

Ndugu hawa wanasema kuwa kiwango hicho ni cha chini sana kushinda pesa aliyolipa wakati alikana mashtaka ya kuua.

Familia ya Ismael ilifika katika kituo cha polisi Rabai kuonyesha kero kubwa wa kutopata haki.

 Gusa usome hadithi za Abraham Kivuva

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments