Familia Moja Yalilia Haki Baada Ya Mwanao Kugongwa Na Mhudumu Wa Pikipiki Na Kufariki

Familia moja kutoka mjini Webuye inalilia haki baada ya mwanao wa kike mwenye umri wa miaka tisa  kugongwa na mhudumu mmoja wa pikipiki na kufariki katika eneo la Makhese huku polisi wakishindwa kumfungulia mashtaka mhudumu huyo

Kulingana na Nasimiyu Wekesa mamake marehemu inadaiwa kuwa mwanawe aligongwa mwezi uliopita na kufariki akipelekwa hospitalini na licha ya polisi wa trafiki aliyekuwa eneo la tukio hilo kumukamata mshukiwa na kuenda naye katika kituo cha polisi mjini Webuye mshukiwa huyo aliachiliwa na hajafunguliwa mashtaka hadi kufikia  sasa

Sasa mama huyo anatoa wito kwa serikali kumsaidia ili haki itendeke na mshukiwa huyo achukuliwe hatua za kisheria

Aidha mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za kibinadamu magharibi mwa kenya Human Rights Watch  Peter Wekesa ametoa wito kwa polisi kuhakikisha kuwa mshukuiwa huyo amekamatwa na kufikishwa mahakamani .

-Brian Ojamaa