Familia na marafiki wa marehemu Ken Okoth waungana pamoja kuadhimisha mwaka mmoja wa kifo chake

Mnamo tarehe,24, Julai Ijumaa jamaa na marafiki waliungana pamoja katika kanisa la katoliki la Our Lady of Guadaloupe mtaa wa Kibra ili kuadhimisha mwaka mmoja tangu mbunge wa Kibra Ken Okoth kuaga dunia.

Kupitia kwenye miyandao ya kijamii ya twitter chama cha ODM kiliposti picha za hafla hiyo na kuandika ujumbe mfupi.

"SG @edwinsifuna aliungana na fa,ilia, marafiki na jamaa za mwendazake Ken Okoth ili kuadhimisha mwaka mmoja tangu afariki,  kabla ya kifo chake Okth alikuwa mbung wa Kibra

Hafla hiyo ilifanyika katika kanisa la katoliki la Our Lady of Guadaloupe, Kibwa." Chama cha ODM kilinakili.

https://twitter.com/TheODMparty/status/1286714813998141440

Katibu mkuu wa chama hicho ODM Edwin Sifuna alikuwa na haya ya kunakili,

"Leo tuko katika kanisa la Our Lady of Guadaloupe, Kibra ili kumkumbuka marehemu Ken Okoth na kuadhimisha mwaka mmoja tangu atuache  Shine on your way bro. #MbelePamoja."

Mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Kiranyaga Wangui Ngirici naye alijiunga na familia ili kumkumbuka mwendazake

“Today I join Kenyans in celebrating the first anniversary of the late Hon. Ken Okoth. This nation will always preserve his great legacy & if there’s a mantra Mheshimiwa left behind is that ;There’s Honour In serving Wanjiku." Aliandika Wangui.

Hizi hapa baadhi ya picha za hafla hiyo;