Familia ya Oprong yaomba msaada wa mazishi

oduya-pic
oduya-pic

Familia ya aliekuwa mbunge wa kwanza wa eneo la Teso siku hizo likijulikana kama Busia kaskazini Oduya Oprong imetoa wito kwa serikali kuisaidia kumzika mbunge huyo mbali na kuwasaidia wanao na wake zake ambao wanaishi maisha ya ufukara.

Wanafamilia hiyo wakiongozwa na kasisi George Etyang na Abel Okerogei wanasema kwa sasa hawana uwezo wa kugaramia mazishi ya mbunge huyo ambaye kwa wakati mmoja alikuwa naibu waziri wa mipango.

Wito wao umeungwa mkono na wabunge Raphael Wanjala wa Budalangi, John Bunyasi wa Nambale na mbunge mwakilishi wa akina mama kaunti ya Bungoma Catherine Wambilianga.

Aidha wamemtaja marehemu Oprong kama mfalme wa jamii ya Iteso ambaye aliisaidia pakubwa hasa katika kusajiliwa kwao na kutambulika na serikali ya Kenya kama moja ya jamii za humu nchini.