Familia Yalilia Haki Baada Ya Binti Yao Kubakwa Na Kupewa Mimba Na Baba Wa Kambo

kubakwa
kubakwa
Familia moja kutoka eneo bunge la Tongaren kaunti ya Bungoma inalilia haki baada ya mwanao wa miaka kumi na minne kubakwa na kupachikwa mimba na babake wa kambo.

Vincent Wanyonyi ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Mwibale anadaiwa kumtendea unyama huo bintiye wa kambo mwaka jana mwezi wa Oktoba aliporejea nyumbani kutoka shuleni ili kupokea matibabu baada ya kuwa mgonjwa.

Msichana huyo aliyekuja na mamake kwa ndoa hiyo pindi tu mamake alipooleka kama bibi wa pili kwa Wanyonyi, alielezea jinsi babake wa kambo alimlazimisha kufanya ngono naye alipokuwa mgonjwa akiwa amelala kitandani wakati mamaye alikuwa ameenda sokoni.

Kwa sasa mamake na familia hio inataka mwalimu huyo achukuliwe hatua kali za kisheria.

-Brian Ojamaa