FARE THEE WELL :Soma ujumbe wa mwisho wa Miguna Miguna kwa marehemu baba mkwe wake

  Wakili  Miguna Miguna ameandika ujumbe  wneye hisia wa kumkumbuka baba  mkwe wake baada ya kukosa kuhudhuria maazishi yake . Benson Awange alifariki januari tarehe mbili mwaka huu katika kaunti ya Migori .Juhudi za miguna kutaka kuja nchini ili kuhudhuria maazishi yake zimegonga mwamba  baada ya mahakama kuahirisha kesi yake hadi tarehe 23 machi .Baada ya kushindwa kufika katika maazishi hayo Miguna aliutuma ujumbe huo wa kumbukumbu kwa  baba mkwe wake .

" Naomba radhi mzee   Omolo Awange  kwa mimi kutoweza kufika ili kuhudhuria maazishi yako hata kwa lazima .Lakini nipo hapa nawe . Nafsi yangu ipo hapa nawe’ aliandika Miguna . Alimtaja baba mkwe wake kama mtu aliyependa kusoma  kila aina ya vitabu  pamoja na magazeti ."Mzee Molo Awange  alisoma vitabu vyoye nilivyochapisha  na makala nilioandika magazetini .Pia alifuatilia kwa karibu shughuli zangu zote katika vyombo vya habari’.

  Pia alimshuru baba mkwe wake kwa kumruhusu awe mume wa binti yake kwa  miaka 20. Aliahidi kuendelea kupigania haki zake na hatosalimu amri . Wakili wake John Khaminwa atawasilisha rufaa dhidi ya uamuzi wa kuisongesha mbele kesi yake hadi tarehe 23 machi . Khaminwa amesema mteja wake, Miguna  anapitia mahangaiko huko ulaya .