Ferdinand Waititu kukabiliana na seneti jumanne wiki ijayo

Ferdinand Waititu anatarajiwa kufika mbele ya seneti wiki ijayo jumanne ili aweze kujitetea kwa mashtaka aliyokuwa amedaiwa kufanya na mahakama.

Gavana huyo alishtakiwa kwa kupatikana na ufisadi na kisha kukatazwa na kuzuiwa kufanya kazi katika ofisi yake na alikana makosa hayo.

Spika wa seneti Kennedy Lusaka aliliambia gazeti la the star kuwa siku za usoni za gavana Waititu sasa ziko mikononi mwa seneti.

"Tutawaskiza tarehe, 28 na 29 kisha tutaweka mjadala na mwishowe tutaweza kupiga kura," Lusaka alisema.

Maseneta ambao wanaunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kutokana na agenda ya BBI wanataka gavana huyo atolewe katika ofisi ilhali wafuasi wa naibu rais William Ruto wanapigana ili Waititu aweze kusalia ofisini.

Jumatano maseneta wa Kieleweke waliweza kukabiliana na maseneta wa ODM na kuandaa mjadala motomoto na kuzungumzia kama wanaweza kutenga kamati maalum ili kuchunguza mashtaka hayo ambayo yalipingwa.

Waliweza kupiga kura 28 kwa 15 kwa kutilia mkazo mjadala ambao kiongozi wa wengi Kipchumba Murkomen aliweza kutoa na kusema kuwa kamati maaalum iweze kuteuliwa kwa ajili ya kesi hiyo.

Kieleweke iliweza kudai kuwa kamati ambao walikuwa wanaunga mkono walikuwa wanamsaidia waititu.

"Siasa ni mtizamo kwa hivyo tuweze kubadilisha orodha ili wanakamati wenzetu(kieleweke) waweze kusikia wamo na ujasiri," Seneta Farhiya Ali alisema.

Katika sehemu ya 33 (7) ya kaunti ya serikali inasema kuwa, kama maseneti wengi wataweza kushikilia mashtaka ya uongo kwa hivyo  gavana ataweza kushikilia ofisi yake.

Hii ina maana kuwa angalau maseneta 24 kwa 47 wanahitajika kupiga kura ili waweze kumtoa gavana Waititu katika mamlaka.

Kwa sasa chama cha Jubilee kimeweza kuwa na kaunti 27 ilhali Nasa imeweza kuwa na kaunti 20, maseneta ambao wamo katika kikundi kile kingine ni pamoja na Irungu Kangata, Kimani Wamatangi, Johnson Sakaja, Emphraim Maina na Gideon Moi.

Mashtaka ya wabunge wa Kiambu ilisema kuwa hakukuwa na uajibikaji wa mali za umma na mali ya kaunti na kusababisha deni kubwa  la billioni nne katika kaunti ya Kiambu.

"Gavana aliweza kutumia pesa za uma za miradiya kaunti kwa kifanyia mambo yake yasiyostahili," Hati ilisoma.

Walioshtakiwa na gavana huyo ni pamoja na mke wake Gavana na washukiwa wengine nane.