Serikali aidha imependekeza kuwa tarehe 25 Mei mwaka huu ambapo itakuwa Jumatatu kuwa siku ya kitaifa kwa maadhimisho ya siku japo ikawarai waumini wa dini hiyo kusherehekea nyumbani kama njia ya kuzuia watu kutangamana eneo moja.
Alhamisi, kamati kuu ya miungano ya waislamu nchini ilisema serikali ni sharti ifungue misikiti akisema wana uwezo wa kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali.
“If the government can trust drunkards enough to keep social distancing in eateries, then it should trust Muslims enough to open mosques for Idd prayers,” amesema Sheikh Juma Ngao.
Sheikh amesema ni kinaya kuwadhamini watu walevi kwa kufungua maeneo ya burudani na kuendelea kufunga misikiti nchini.
na azimio la serikali la kutaka watu kuwa umbali wa kilomita moja
Ameongeza kuwa kaunti kama vile Kwale, Marsabit, Meru, Kisumu na Lamu zote zimesajili visa vichache vya maambukizi ya virusi hivyo.
Ametilia mkazo kuwa misikiti ambayo haitazingatia masharti yaliyowekwa na serikali ni sharti ifungwe .