FIMBO YA MZEE MOI YAONEKANA: Rungu ya Hayati Mzee Moi haijaachwa nyuma

 Kirungu kidogo ambacho   rais mstaafu Daniel Moi  alifahamika sana kwa kutembea nacho pia kimepelekwa bungeni ambako mwili wake umewekwa ili kutazamwa na wakenya .

Moi  hakuwai kuzungumza kuhusu umuhimu wa rungu hiyo  lakini chimbuko la kuwa nayo ni kutoka jamii yake ya Tugen   huko Baringo ambapo vijana hushauriwa na wazee kutemebea na angalau silaha ya kujilinda dhidi ya wanyama wa msitu ." Kuanzia akiwa mdogo ,Moi alikuwa akijihami kwa rungu ,mshale au kisu ili kujilinda dhidi ya wanyama hatari kama vile Chui  , sokwe au  mwewe ‘ Ameandika  Andrew Morton aliyeandika  wasifu wa  Mzee Moi   kwa jina -Moi, the Making of an African Statesman'',  kitabu ambacho kilichapishwa mwaka wa 1998 .