Wakati mkutano huo ,Sakaja amesema kundi la wajenzi wa barabara na vifaa vyao tayari vimetumwa katika eneo hilo na hatua zaidi zitafuata . Hatua ya Sakaja kuingilia kati imejiri baada ya maandamano ya siku nne ya wahudumu wa matatu wanaoitumia barabara hiyo ambao wamekuwa wakilalamikia hali mbaya ya barabara hiyo . Tangu jumatatu wahudumu hao ambao wamechoshwa na visa vya kila mara vya kuharibika kwa magari yao waliizaba barabara hiyo na nyingine zinazoelekea katika barabara kuu ya Thika .
Wakaazi wa mtaa huo wamelazimika kutembea kwa wiki nzima hadi Roysambu ambako wamechukua matatu za kwuafikisha katikati mwa jiji . Hali mbovu ya barabara ya Kasarani kwenda Mwiki imekuwa kidinda sugu kwa wenyeji na maanadamano hayo sio mapya kwani yalianza hata wakati ya serikali za mabaraza ya miji kabla ya kuja kwa mfumo wa ugatuzi . Serikali ya kaunti ya Nairobi chini ya utawala wa Evans Kidero ilitumia shilingi milioni 500 kuifanyia ukarabati barabara hiyo lakini baada ya miezi kadhaa wakaazi walirejelea maandamano kwa sababu ya kurejea kwa mashimo katikati ya barabara .