Abike Dabiri-Erewa, mwenyekiti wa jamii ya wanigeria walioko nje ya nchi amesema Kafayat Amusan alimzaa mtoto wa kiume dakika 30 baada ya ndege kuondoka uwanja wa ndege. Ndege hiyo ililazimika kurejea Dubai ili kuhakikisha kwamba mama na mtoto wapo salama .
Amusan na mwanawe wapo katika hali nzuri kiafya na wamelazwa katika hospitali moja Dubai. Wanatarajiwa kurejea Nigeria pindi cheti za kuzaliwa cha mtoto huyo kitakapotolewa na stakabadhi nyingine za usafiri kutayarishwa. Mwanamke huyo alikuwa katika kundi la kwanza la raia wa Nigeria waliotolewa UAE kurejeshwa nyumbani kwa sababu ya janga la virusi vya Corona .
Watu 256 waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Muhammed jijini Lagos Jumatano saa moja jioni. Maamlaka za Nigeria zimesema zimefaulu kupata sehemu ambazo raia wake wanaorejea watakapotengwa katika karantini.