Fomu mbaya ya United yaendelea baada ya kubwagwa na Burnley

burnley
burnley

Fomu mbaya ya Manchester United iliendelea jana walipopoteza 2-0 nyumbani, kwa Burnley. Burnley waliongoza kabla tu ya muda wa mapumziko wakati Chris Wood alipofunga bao.

Jay Rodriguez kisha akaongeza bao la pili na kuwapa ushindi wao wa kwanza Old Trafford. United walizomewa wakati wa mapumziko na baada ya mechi kuisha huku mashabiki wakiondoka uwanjani ikiwa imesalia dakika tano mechi kutamatika.

Manchester United huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes kwa mkataba wa pauni milioni 55m mwisho wa wiki hii baada ya kuafikiana na Sporting Lisbon.
Fernandes aliwapuuza mashabiki wa Sporting na kusukuma kamera za televisheni baada ya kupoteza mechi dhidi ya Braga siku ya Jumanne katika kile kilionekana kuwa mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo.

Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 13 katika mechi 10 alizocheza Juventus walipowanyuka AS Roma 3-1 na kufuzu kwa nusu fainali ya Coppa Italia. Mshambulizi huyo wa Ureno alianza kufunga kunako kipindi cha kwanza kutoka kwa pasi ya Gonzalo Higuain. Rodrigo Bentancur na Leonardo Bonucci kisha wakaongeza mabao mengine na kufanya mambo kuwa 3-0 kabla ua muda wa mapumziko. Roma ilipata boa lake kupitia kwa Cengiz Under.

Juventus watakabana na aidha AC Milan au Torino kwenye nusu fainali.

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeialika Libya kushiriki katika michuano ijayo ya fainali za ubingwa wa mataifa Afrika huko Cameroon.

Caf wanatafuta timu itakayochukua nafasi ya Tunisia, ambao wamejiondoa kutoka kwa kipute hicho, baada ya vilabu vya nchi hiyo kudinda kuwawachlia wachezaji wake. Wanahoji kuwa mishuano hio haiku katika kalenda rasmi ya FIFA na kwa hivyio wanataka kulinda afya ya wachezaji wao.

Cameroon au Ivory Coast haitashiriki katika kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar baada ya timu hizo kuwekwa katika kundi moja kwenye raundi ya pili ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia. Indomitable lions imewakilisha Afrika mara saba katika kombe la dunia, huku Ivory Coast ikishiriki katika kombe hilo mara tatu.

Ghana na Afrika Kusini zitakutana katika kundi G pamoja na Zimbabwe na Ethiopia huku Misri na Angola pia zikikutana katika kundi F pamoja na Gabon na Libya.

Misri ilikuwa miongoni mwa wawakilishi watano wa Afrika katika kombe la dunia pamoja na Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia na zote zinaamini kwamba zina fursa nzuri ya kufika katika raundi ya tatu na ya mwisho mnamo mwezi Novemba mwaka huu.

Takriban pauni bilioni 7.35 zilitumika katika uhamisho wa wachezaji soka wanaume mwaka wa 2019, kulingana na ripoti ya FIFA. Kiwango hicho kimeongezeka kwa asilimia 5.8 mwaka wa 2018 za uhamisho kote duniani.

Vilabu vya Uingereza vilitumia pauni bilioni 1.5 ambalo ni punguzo la asilimia 11 kutoka mwaka 2018, huku kukiwa na ongezeko la asilimia 16 kwa kiwango kilichotumika kwa uhamishi wa wachezaji wa kike.