logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Junior Starlets kucheza mechi ya kwanza ya kombe la dunia usiku wa kuamkia Ijumaa

Timu ya taifa la Kenya ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 17 itaanza safari ya kombe la dunia dhidi ya Uingereza

image
na Brandon Asiema

Football17 October 2024 - 10:51

Muhtasari


    Baada ya ngoja ngoja hatimaye kwa mara ya kwanza katika historia ya kandanda nchini Kenya, timu ya taifa itashiriki kombe la dunia kwa kucheza mechi yake ya kwanza Ijumaa 18, dhidi ya Uingereza mwendo wa saa 8 usiku majira ya Afrika Mashariki.

    Kenya inawakilishwa na timu ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 17 chini ya kocha Mildred Cheche kwenye kipute hicho kinachoandaliwa katika nchi ya Jamhuri ya Dominican.

    Vipusa hao wa Kenya walifuzu kushiriki kombe la dunia makala ya mwaka huu kwa kuicharaza Burundi mechi za mkondo wa kwanza na mkondo wa pili kwa jumla ya magoli 5 kwa nunge.

    Barani Afrika, timu za taifa za Kenya, Nigeria na Zambia zilifuzu kombe hilo la dunia.

    Mechi za ufunguzi katika makundi mbali mbali zilichezwa Jumatano 16.

    Wawakilishi wa Afrika Nigeria waliwashinda New Zealand kwa mabao 4 kwa moja huku Uhispania wakiwatia darasani Maerekani kwa ushindi wa mabao 3 kwa moja.

    Mechi kati ya Colombia na Korea Kusini iliishiwa kwa sare ya kufungana bao moja kwa moja, wenyeji Jamhuri ya Dominican wakikubali kichapo cha mabao 2 kwa nunge.

    Wawakilishi wengine wa bara la Afrika Kenya watacheza dhidi ya Uingereza Ijumaa saa nane usiku wenzao Zambia wakimenyana  na Brasil wakati huo.

    Kenya ipo katika kundi moja na Uingereza, Korea Kaskazini na Mexico.



    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved