Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza Morocco
kuwa mwandalizi wa fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa wanawake Makala
ya mwaka huu.
Nchi ya Morocco iliwahi kuandaa mashindano hayo mwaka wa 2022 ambapo timu ya ASFAR kutoka nchi hiyo ilinyakua taji hilo mwaka huo baada ya kuishinda Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Timu sita zilifuzu kushiriki ligi hiyo kutoka kwa miungano minane ya soka kwa kuzingatia maeneo kigiografia katika michuano ya mchujo.
Mamelodi Sundowns walifuzu moja kwa moja kama mabingwa watetezi huku ASFAR wa Morocco wakifuzu kutokana na kuwa waandalizi wa kipute cha mwaka huu.
Katika ukanda wa Afrika mashariki na kati chini ya muungano wa CECAFA, timu ya wasichana ya CBE FC kutoka Ethiopia ilifuzu kushiriki klabu bingwa barani upande wa wanawake baada ya kuilaza Kenya Police Bullets FC katika fainali ya michuano ya kufuzu makala ya mwaka huu.
Timu nyingine kutoka CECAFA zilizowai kushiriki mashindano
hayo ni Vihiga Queens ya Kenya katika mwaka wa 2021, Simba Queens ya Tanzania
mwaka wa 2022 na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ta Tanzania katika mwaka wa 2023.