logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Taaluma ya Austine Oduor Origi katika timu ya Gor Mahia

Austine alianguka na kuaga akiwa nyumabni kwake katika eneo la Mumias.

image
na Brandon Asiema

Football17 October 2024 - 09:16

Muhtasari


  • Austine alichezea klabu ya Gor Mahia sawia na timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars ambako alikuwa nahodha kwa timu hizo mbili.


Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Gor Mahia na Harambee Stars Austin Oduor maarufu kama Makamu, aliaga dunia Oktoba 16.


Beki huyo maarufu, alijiunga na Gor Mahia mwaka wa 1980 akitokea Luo Union.


Katika taaluma yake ya soka ya zaidi ya miaka 10, Makamu ameshinda mataji mengi akitumikia timu hiyo, ikiwemo mataji ya bara Afrika na taji ya ligi kuu nchini.


Aidha katika timu ya taifa, Austin Oduor atakumbukwa katika michuano ya kufuzu AFCON ya mwaka 1990 akiwa nahodha wa Harambee Stars. Katika mchuani huo, Oduor alipewa jukumu na kocha wake Mohammed Kheri kuhakikisha mshambuliaji anayekisiwa kuwa bora zaidi barani Afrika George Wear wa Liberia hapati nafasi ya kufunga bao.


Akiongoza wachezaji wenzake uwanjani kama nahodha, Harambee Stars waliwafunga Liberia bao moja kwa nunge katika mchunuano wa kundi lao lililojumuisha timu za taifa za Liberia, Egpyt na Malawi.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved