logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Thomas Tuchel afunguka kwa nini alikubali kazi ya umeneja wa Uingereza na sio Man United

Mjerumani huyo alikuwa amehusishwa sana na kuchukua mikoba ya ten Hag ambaye amekuwa na mwanzo mbaya katika United.

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Football17 October 2024 - 08:27

Muhtasari


  • Kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 kutoka Ujerumani alisema kukubali kazi ya Uingereza ulikuwa ni uamuzi wa wazi wa moja kwa moja licha ya ripoti kumhusisha na Mashetani Wekundu.
  • Kuthibitishwa kwa Tuchel kama kocha mpya wa Uingereza kulikuja zaidi ya wiki moja baada ya kuripotiwa kuwa Mjerumani huyo alikuwa amepangwa kuchukua nafasi ya Erik ten Hag

Licha ya kuhusishwa sana na kazi ya ukocha wa Manchester United, bosi wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich Thomas Tuchel mnamo siku ya Jumatano alitangazwa kuwa meneja mpya wa timu ya taifa ya Uingereza, akichukua mikoba ya Gareth Southgate aliyeondoka mapema mwaka huu.

Katika mahojiano na waandishi wa habari, kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 kutoka Ujerumani alisema kukubali kazi ya Uingereza ulikuwa ni uamuzi wa wazi wa moja kwa moja licha ya ripoti kumhusisha na Mashetani Wekundu.

Tuchel aliwaambia waandishi wa habari kuwa alivutiwa na mtazamo wa Shirikisho la Soka la Uingereza alipokuwa akieleza kwa nini alishawishika kuchukua kazi ya kunoa Three Lions.

"Wazo na jinsi John [McDermott, mkurugenzi wa ufundi] na Mark [Bullingham, mtendaji mkuu] waliliwasilisha lilikuwa la haraka sana na la siri. Lilikuwa la moja kwa moja, lilikuwa uamuzi wa kazi hii na sio dhidi ya kitu kingine chochote," Tuchel alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Aliongeza, "Waliweka wazi kuwa ni kuhusu mpira wa miguu na hilo lilinifurahisha. Sikuwa na uhakika kwamba hii ilikuwa kazi yangu kwa sababu ratiba ni tofauti sana. Siku zote nilitaka kurudi Uingereza, hilo lilikuwa lengo langu kubwa. Ofa ilikuja kwa wakati ufaao na tulipata maono ya kushiriki. Sasa sina budi kuishi kulingana nayo. Najua kuna mataji na ninataka kusaidia hilo kutokea."

Tuchel alithibitishwa kuwa meneja ajaye wa kudumu wa England siku ya Jumatano baada ya kufikia makubaliano na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) kwa kandarasi ya miezi 18.

Kuthibitishwa kwa Tuchel kama kocha mpya wa Uingereza kulikuja zaidi ya wiki moja baada ya kuripotiwa kuwa Mjerumani huyo alikuwa amepangwa kuchukua nafasi ya Erik ten Hag katika klabu ya Man United.

Ten Hag yuko chini ya shinikizo kwa mara nyingine tena huku United ikiwa na mwanzo mbaya wa msimu huu na inasemekana wakurugenzi wa klabu wamejadili uwezekano wa kumnunua Tuchel.

Tuchel sasa ataanza rasmi kukinoa kikosi cha Uingereza Januari mwaka ujao.

Kabla ya hayo, Lee Carsley atasalia kama meneja wa muda kabla ya kurejea katika nafasi yake kama mkufunzi wa timu ya vijana ya chini ya miaka 21 ya England.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved