logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Junior Starlets wafungua michezo ya kombe la Dunia kwa kipigo dhidi ya Uingereza

Kocha wa Junior Starlets bado ana matumaini licha ya kufungia udhia na kibano cha 2-0 mikononi mwa Uingereza

image
na jacob kimanthi

Football18 October 2024 - 08:11

Muhtasari


  • Junior starlets wazabwa mabao 2-0 na Uingereza katika mechi ya Ufunguzi kundi C.
  • Junior Starlets watacheza na Korea ambao walimchakaza Mexico mabao 4-1 kabla ya kumalizia mechi ya makundi na Mexico.

Timu ya kina dada wasiozidi umri wa miaka kumi na 17, Junior Starlets ambao walifanya vizuri katika juhudi za kutafuta nafasi ya kushiriki katika kipute cha kombe la dunia, walifungua michezo hiyo kwa kibano cha mabao 2-0 mikononi mwa young lioness wa Uingereza katika mechi ya ufunguzi kundi C.

Kombe hilo ambalo limeandaliwa katika taifa la Dominican Republic liling'oa nanga mnamo tarehe 16 Oktoba linatarajiwa kushika kasi huku mechi za makundi zikiendelea.

Starlets katika mchezo huo walionyesha umahiri na kutulia kwingi licha ya kuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki katika ngazi hii.Valarie Nekesa alionekana kuwatatiza mabeki wa timu hii ya Uingerza lakini shuti lake kunako dakika ya tatu ya mchezo ilikuwa hafifu mno na kuelekea moja kwa moja mikononi mwa mlinda lango wa timu pinzani Hope McSheffrey.

Timu ya Uingereza ambao wa uzoefu na kuimarika kwingi kwenye ngazi hii walionekana kumilisi sana mchezo kipindi cha kwanza huku mawing'a wa Uingereza wakiongoza na  Lola Brown na Erica Parkinson walikuwa tishio lakini safu ya ulinzi ya Kenya ilibakia imara zaidi na kuwanyima nafasi mwafaka ya kupachika bao kimyani.

Licha ya kuwa imara, kunako dakika ya 28, Uingereza walifanikiwa kupata mkwaju wa penati uliosababishwa na makosa ya beki Diana Anyango baada ya kuunawa mpira, na ambako shuti la mchezaji anayechezea timu ya Chelsea Lola Brown lilimshinda kasi mlinda lango Velma Abwire na kuzama wavuni.

Kunako kipindi cha pili,kocha wa Starlets Mildred Cheche alifanya mageuzi ya kuwaleta nguvu wapya mchezoni ndiposa kudhibiti joto la mchezo kutokana na mashambulizi ya kila mara kutoka kwa Uingereza.

Katika dakika nne kipenga cha mwisho kupulizwa, Uingereza walifanikiwa kupata bao lingine na la pili.Bao hilo lilifungwa na nguvu mpya upande wa Uingereza Lauryn Thompson na kuwahakikishia Uingereza pointi zote tatu.

Licha ya kupoteza pambano hilo kocha Mildred Cheche alionekana kutulia na kujawa mna matumaini kwani Starlets walicheza vizuri katika pambano hilo na kuonyesha matuimaini ya kuandikisha matokeo mazuri katika mechi zijazo katika kipute hicho.

Katika mechi nyingine ambayo ilichezwa sawia kwenye kundi hilo ni kwamba timu ya Korea na ambao ni washindi mara mbili wa kipute hiki waliwapiku wanadada wa taifa la Mexico mabao 4-1 ambako mchezaji Choe Rim Jong alifunga mabao matatu ikiwa ndio yakwanza katika kipute hiki kutoka kwa mchezaji mmoja.

Baada ya kipigo hicho sasa Starlets watakabana koo na timu ya Korea kabla kumalizia mechi za makundi na timu ya Mexico.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved