Free! Wachezaji 2 wa Raga walioshtakiwa kwa ubakaji waachiliwa kwa dhamana

Wachezaji wawili wa raga walioshtakiwa kwa kumbaka mwanamke mmoja mwaka wa 2018 wameachiliwa kwa dhamana ya  shilingi laki tatu pesa taslimu na  hakimu wa  Zainab Abdul.

Alex Olaba (23)  na  Frank Wanyama (22)  waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela  walipata afueni baada ya mahakama  kuagiza washtakiwe upya Juni tarehe 30.

Walipewa hukumu hiyo na hakimu mkuu Martha Mutuku  Agosti mwaka jana. Mutuku alikuwa amewapata na hatia ya ubakaji.

Walishtumiwa kwa kumbaka mwanamke huyo ambaye ni mwanamuziki mwaka wa 2018 katika karamu moja  mtaani Highrise.