FREE:Mahakama yawapata bila hatia washukiwa 9 wa mkasa wa Bwawa la Solai .

SOLAI
SOLAI
Mahakama   ya  Naivasha imewapata bila hatia ya mauaji ya kutokusudia washukiwa tisa  walioshtakiwa kwa mkasa wa bwawa la Solai uliosababisha vifo vya watu 48  miaka miwili iliyopita .  Hakimu mkuu wa Naivasha Kennedy Bidali  amewaachilia tisa hao huru kwa sababu ya ukosefu wa ‘nia ‘ ya afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma   kutoa ushahudi na msaada wa kuwashtaki tisa hao .

Dakika chache baada ya uamuzi huo kutolewa ,washukiwa akiwemo Perry Manusukh Kanasagara,  mmiliki wa shamba husika  na maafisa kadhaa wa serikali walionekana wakitabasamu baada ya kungoja kwa uamuzi kwa muda mrefu .

Kwa upande mwingine ,manusura wa mkasa huo  wakiwemo maajuza  waliokuwa wamepiga kmabi kortini tangu kesi hiyo kuanza waliachwa na majonzi wakitafakari hatua ifuatayo . Hakimu ameilaumu afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma  akisema miezi kadhaa tangu kesi hiyo kuanza ,imekuwa ikiahirishwa kila wakati . Bidali ameishtumu afisi ya DPP kwa kuiteka nyara mahakama kwa kudinda kufika kortini .