Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ijumaa alifunguka kuhusu uhusiano wake spesheli na marehemu gavana wa Bmet Joyuce Laboso .Laboso, kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2013 alikitema chama cha Raila ODM na kujiunga na mrengo wa naibu w arais William Ruto wa chama cha URP ambacho kilikuwa kimeteka siasa za Rift valley . Alikitetea kiti chake cha ubunge cha Sotika ,hatua ambayo wengi wanasema ni kwa sababu ya hadhi yake ,uadilifu na rekodi nzuri ya maendeleo . Raila amesema ilikuwa vigumu sana kwa yeye na Laboso kuzungumza wakiwa nchini kenya kwa sababu walikuwa katika vyama pinzani ."Laboso alishinda kiti cha Sotik lakini ilikuwa vigumu sana kwa sisi kuzungumza kwa sababu alikuwa katika chama hasimu’ amesema Odinga wakati wa misa ya wafu ya Bi Laboso iliyofanyika katika uwanja wa Bomet .
Balozi huyo wa umoja wa mataifa amesema walitangamana kwa muda na Laboso wakati wa kongamano la chama cha Democratic nchini Marekani mwaka wa 2016 .Raila alimtaja Laboso kama binti yake kwani alikuwa kielelezo kwake na mara nyingi Laboso alitaka ushauri wa kisiasa kutoka kwake . Kiongozi huyo wa ODM alifichua kwamba siku moja alimwambia Laboso kwamba angekuwa rais wa Kenya .
" Siku moja ,naona ukitoa hotuba kama rais wa kenya . nchini Kenya hatuwezi kuzungumza kwa kina lakini hapa tunaweza kuongea’ Raila alimwambia Laboso walipokuwa Marekani .Joyce aliaga dunia siku ya jumatatu katika Nairobi Hospital baada ya kupambana na kwa muda mrefu na ugonjwa wa kanasa . Mwili wake umesafrishwa hadi Fort Tenan ,Kisumu kwa maazishi ,Jumamosi .