Game Kali ? Nalipwa shilingi 500,000 kila mwezi na baba za watoto 6 niliiozaa na wanaume tofauti matajiri

esther
esther
Esther* anafahamika mtaani kama  mama ‘international’ kwa sababu ana watoto wawili wazungu  waliozaliwa na baba tofauti na  watoto wengine  wane waliozaliwa na wanaume tofauti wenye pesa katika ulingo wa kisiasa ,kibiashara na mabalozi .

Sifa zake hata hivvyo iso kuhusu uraia wa watoto wake bali alichofaulu kufanya ili kuwa na wanawe na maisha ambayo sasa anaishi kama malkia bila kufanya kazi . Esther hajawahi kugharamika hata kwa shilingi kuishi maisha yake ya kifahari kwa sababu baba za watoto wake hutuma pesa kila mwezi kwa matumizi ya wanao kuanzia karo ya shule ,  usafiri,kodi ya nyumba na chakula .kwa mwezi ,imedaiwa kwamba Esther hulipwa takriban shilingi nusu milioni na endapo kila baba ya mtoto wake angewajibika kwa kutuma pesa ,mwanamke huyo angekuwa akiingiza kitita cha shilingi milioni 1 kwa mwezi kama pesa za matumizi .

Sarakasi  zake  na wanaume zilianza alipkuwa akifanya kazi katika ubalozi mmoja  wa taifa la kigeni na akiwa huko alijipata katika uhusiano wa kimapenzi na mfanyikazi mwenzake ,mzungu ambaye baadaye walipata mtoto naye na jamaa akarejea kwao . Licha ya kuachana  mzungu huyop aliendelea kuwasiliana naye na hata alipojifungua jamaa alizidi kutuma pesa za matumizi ya mwanawe .Hapo ndipo Esther alipopata ujanja wa kuweza kupata pesa maisha yake yote bila kwenda kazini .

Kwa sababu ya  kazi yake alikuwa akikutana na watu mbali mbali wengi raia wa kigeni katika balozi nyingine na muda sio mrefu ,alikuwa tena kapatana na mzungu wa taifa jingine ,kamuingiza boksi na kaboom! Alipata tena uja uzito na akazaa mwanawe wa pili .mzungu wa pili pia kaanza kutuma pesa na hapo ndipo Esther alipopata ujasiri wa kuzaa na wanaume wengine lakini wakenya waliokuwa pia na uwezo wa kifedha kugharamia mahitaji ya watoto wao kama walivyokuwa wakifanya wale wazungu.

Kamwe hakuolewa wala kuingia katika uhusiano wa wazi na yeyote  kati yao lakini alizidi kuwatumia watoto kama chambo cha kuzidi kuvuna pesa kutoka kwa baba za watoto  wake .

Magari anayobadilisha kila mara na ziara za holiday anazopiga Esther huwezi kuzimudu iwapo huna  bunda la kutosha la mihela ,wengi  wasiojua mchezo wake hata walimshuku kuwa muuzaji wa mihadarati lakini siri  yake ilipogunduliwa ,Esther hakuwa na soni kwa sababu  alionekana kufurahia maisha yake na mtindo  aliochukua nao wanaume wale walifurahi kuendelea kugharamia maisha ya watoto wao ambao walikuwa chini ya paa moja . Dunia ina mambo!