Nigeria team

Gani Kali? Mechi tatu za AFCON zinapigwa leo

 Mechi za  kombe la Afcon zinaingia siku ya sita leo  huku michuano mitatu ikitarajiwa kupigwa .Mchuano wa kwanza utahusisha  the super Eagles ,Nigeria ikizichafua dhidi ya Guinea . Nigeria ilianza vyema mechi hizo baada ya kuilaza Burundi bao moja kwa nunge katika mechi yao ya kwanza .Lakini wengi wanajiuliza iwapo the Super Eagles watayaacha nje ya uwanja masaibu na mgogoro wa malipo ya bonsai ili kupata alama tatu dhidi ya Guinea. Timu ya Nigeria  inalumbana na shirikisho la soka nchini humo kuhusu malipo ya bonasi ya dola 10,000 kila mmoja .

Wakenya hawapaswi kufikiria Tanzania ni timu ovyo – Ghost Mulee

Shirikisho la NFF linataraji kwamba manung’ununiko hayo ya malipo hayatamwagika uwanjani wakati wa mechi yao leo dhidi ya Guinea mwendo wa saa kumi na moja unusu .

Mechi nyingine zitashuhudia  Uganda dhidi ya Zimbabwe mwendo wa saa mbili usiku . Wenyeji Misri  wana kibarua dhidi ya DR Congo  saa tano usiku na wanatafuta ushindi wa pili baada ya kuishinda  Zimbabwe bao moja kwa nunge katika mchuano wao wa ufunguzi .

Tupe ubashiri wako kuhusu timu zitakazosajili ushindi  leo .

 

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments