Gari, Miili ya Mariam Khagenda na mtoto yatolewa, nyufa za serikali zatajwa

unnamed__1570804730_20119
unnamed__1570804730_20119
Ulegevu wa serikali wa kutatua majanga yanayotendeka baharini sasa yameonekana waziwazi.

Nyufa hizi zimejitokeza waziwazi katika operesheni ya siku 13 za kuitoa miili na gari la Mariam Kighenda.

Gari la wawili hawa ilizama majini Sep 30 na imechukua majuma mawili operesheni kumalizika.

Hali ya kupuuza mikakati iliyopo na sheria za usalama katika shirika la feri zimeonekana dhaifu sana.

Soma mengine huku:

Taswira iliyojichora ni taifa na ambalo halina mipangilio mizuri ya kukabili majanga ya ghafla.

Maswali mengi yakiulizwa ni kwa nini serikali imenunua tanki za hewa ya kupumua ya wapiga mbizi hadi mita 30 chini ya baharini wakati na ambapo kivukio cha Likoni kina kima cha mita 60.

Habari hizi zinajiri muda mchache tu baada ya miili ya Miriam  Kighenda na binti yake Amanda Mutheu kupatikana.

Wawili hao walitumbukia katika bahari Hindi Septemba 30 wakati gari walilokuwemo lilipoteleza  kutoka feri na kuanguka baharini.

Soma mengine huku:

Zipo sababu kuu zilizofanya juhudi za kuokoa miili ya mama Kaghenda na mtoto wake Mutheu katika Bahari Hindi kuwa ngumu.

Kwa mujibu wa mpiga mbizi Bassen, Dhoruba kali ya maji ni sababu inayotatiza shughuli hiyo.

Vyanzo vingi vilihoji kuwa huenda gari ya wawili hawa ilipigwa hatua nyingi zaidi na dhoruba hii.

Katika taarifa kwa vyumba vya habari, Bassen alikuwa na imani ya kutegua kitendawili hiki kwa muda mchache baadaye kutokea na kusema kuwa sivyo alivyodhania.

Soma mengine huku:

Presha kubwa ya wakenya ilikuwa kwa jeshi la wanamaji kuutoa mwili huo kabla ya Oktoba 20 siku ya Mashujaa.

Hafla hii itakuwa karibu na eneo hilo la tukio.

Kenya imefanya shughuli hiyo baada ya kutafuta msaada wa wanamaji kutoka Afrika Kusini.