image-2019-01-09(1)

Gathoni Muchomba afichua kilicho wakosanisha na Gavana Waititu (AUDIO)

Mwakilishi wa kina mama katika kaunti ya Kiambu Bi Gathoni Muchomba amekuwa katika vyombo vya habari kwa mda sasa tangia alipochaguliwa mwaka wa 2017.

Kando na kusifiwa kazi anayofanya ya kuwainua kina mama kwa kuwasaidia na mirado yao, alijipata taabani alipopigania nyongeza ya mshahara kwa wajumbe wenzake.

Hata hivyo, uhusiano wake na Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu umedorora huku wawili hao wakijipata wakitofautiana jinsi shughli inafaa kuendeshwa katika kaunti hiyo.

image-2019-01-09(1)

Huku akizungumza na mtangazaji Massawe Japanni, mjumbe huyo alieleza bayana chanzo cha mizozo kati yake na Gavana Waititu huku akidai kuwa wawili hao huzungumza.

Soma usimulizi wake.

Kuna kitu ambacho sijui kama watu wananielewa, watu wengi sana hawanijui labda wananijua tu kwenye redio lakini hawanijui kuwa mtu wa kuongea ukweli.

Mimi siongei ili niwapendeza watu au nisifike mimi huongea ukweli na hiyo style ya kuongea ukweli inanikosanisha na wanasiasa ambao wanapenda siasa ya kuvuma inayo itwa populist politics.

Mimi tulikosana na Gavana, sio personal attack wala ni kikazi kwa sababu mbinu anayotumia kuwasaidia ambao ni walevi sio yenye natumia. Yangu inaitwa medical intervention, yangu lazima upatane na daktari, upewe dawa za kutoa uchofu, upewe chakula cha kujaza mwili na lazima upewe mawaidha ya kiakili.

Mimi naamini mtu anayeshida ya ulevi ni ugonjwa naye Gavana anaamini kuwa aliye na shida ya ulevi ni kukosa ajira. Sasa ukiona tukitofautiana na Gavana ni kwa sababu yeye anataka kwenda kupata walevi, awapatie mia nne wanaenda wanakunywa usiku, kesho wanarudia wanafanya kazi kidogo wanarudi wanakunywa.

Huwa tunaongea ni rafiki yangu tulifanya kampeini pamoja lakini sasa tunatofautiana mbinu ya kufanya kikazi.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments