Gavana Akaranga Alazimika Kuokoa Maisha Ya Mtoto Mwenye Uvumbe Usioeleweka

akaranga
akaranga
Imemlazimu gavana wa vihiga Moses Akaranga kuingilia kati kuokoa maisha ya mtoto Hildah Andisa kutoka kijiji cha navui kaunti ndogo ya vihiga mwenye uvimbe usioeleka huku akiwatia mbaroni mamake Janet Ajima na nyanyake.

Kulingana na jirani yake, mtoto hildah mbaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi ya Navui alianza uvimbe kwenye mguu wa kushoto ulikisiwa kuwa ulikuwa umesababishwa na sindano ya kliniki lakini baadaye kutokeza kidonda kichwani.

Kando ya wazazi kumpeleka hospitalini kubaini kiini cha ugonjwa huo ambao hadi sasa haujaeleweka mtoto huyo amesalia nyumbani mwao huku wazazi wakidai kuwa angepona tu kwa sala.

Gavana akaranga ameelezea kughadhabishwa kwake na hatua ya familia hiyo huku akiwarai wenyeji kutoa habari kwa serikali endapo kutatokea na wangonjwa wa aina yeyote ambao huenda wamekosa matibabu kwa misingi ya mila na itikadi zisozo kuwa na msingi.