Gavana Samboja adinda kupatanishwa na waakilishi wadi

NA SOLOMON MUINGI

Kulikoni Taita Taveta, Gavana Granton Samboja amekataa kata kata kushiriki mazungumzo ya kuleta uiano baina yake na wawakilishi wadi.

Granton SambojaAlisema nia yake ya kutaka kuvunjwa kwa serikali ya kaunti hiyo bado ipo na kwamba anajitayarisha kuwasilisha kwa rais Uhuru Kenyatta zaidi ya sahihi 52,000 zilizochukuliwa kutoka kwa wakazi wa kaunti hiyo. Jopo hilo la wapatanishi linajumuisha kinara wa ODM Raila Odinga na waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa.

Wakati huo huo

Siku moja baada ya waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i kutoa agizo la kufungwa kwa maeneo ya burudani wakati wa zoezi la sensa, kamati ya usalama kaunti ya Taita Taveta imewaonya watakao kiuka agizo hilo. Naibu kamishna wa Mwatate Damaris Kimondo ameagiza machifu wote kuwajibika ili kukomesha unywaji wa pombe haramu vijijini na kutaka ushirikiano kati ya idara ya usalama na jamii.