samboja

Gavana Samboja aponea kubanduliwa

Gavana wa Taita Taveta Granton Samboja amenusurika kutobanduliwa nje katika cheo hicho cha ugavana na wajumbe wa kaunti hiyo.

Kamati ya seneti ambayo ilichunguza misingi ya kubanduliwa kwake kama ilivyopendekezwa na bunge la kaunti hiyo mnamo alhamisi, ilifutilia mbali hoja zilizopitishwa na wajumbe katika kaunti hilo.

Kifo hakichagui!Mpiga picha wa Raila afariki jijini Nairobi

 Wajumbe hao walitaka kumbandua Samboja kutoka mamlakani kwa tuhuma za kukiuka sheria.

Wajumbe 30 ambao walikuwa ndani ya majengo ya bunge waliunga mkono kubanduliwa kwa Samboja.

Harris Keke ambaye ni naibu wa kiongozi wa wengi katika bunge hilo vile vile aliunga mkono kubanduliwa kwa Samboja. Keke alidai kuwa Gavana Samboja alikiuka sheria kwa kutumia vibaya fedha za umma na kuchochea umma dhidi ya bunge hilo.

Kamati hiyo ilisema kuwa madai dhidi ya Gavana huyo hayakuthibitishwa.

Spika wa seneti Kenneth Lusaka aliamua kwamba hakutakuwa na mjadala wowote au kura kupigwa. Hata hivyo aliwapatia washiriki fursa ya kutoa maoni juu ya suala hilo.

”Nilikuwa nalala na wanaume watano.”Binti asimulia kazi ya ukahaba

 

 

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments