Gavana Samboja kufutilia mbali leseni za maduka zinazouza mogoka

Gavana wa Taita Taveta Granton Samboja ametoa amri ya kuzifutilia mbali leseni zote za maduka yanayouza miraa aina ya mogoka kaunti hiyo.

Samboja anasema hatua hiyo imetokana na kilio cha kina mama kuendelea kulalamikia vijana kwa kushindwa na majukumu yao baada ya kujitosa kwa uraibu huo ambao anasema pakubwa unazidi kuathiri maendeleo ya eneo hilo.

Hayo yakijiri, wakazi wa Mariwenyi kaunti ya Taita Taveta wameelezea furaha yao baada ya kampuni ya kuchimba madini ya manganese kuridhi kuwapa ajira watu wasio na ajira katika eneo hilo.

Wanasema kando tu na ajira,kampuni hiyo itasaidia ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.
Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza uchimbaji baadaye kwaka huu.

Kwingineko, mwakilishi wa wadi ya Bunyore magharibi eneo bunge la Emuhaya bw. Manoa Osore amesalia katika njia panda kwa ugavi wa hela kwa vikundi vyakina mama katika eneo hilo.

Hela ambazo walichangiwa na naibu wa rais William Ruto hukubaadhi ya makundi wakitisha donge nono.