Gavana Sephen Sang aachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 1

sTEPHEN Sang
sTEPHEN Sang
 Gavana wa Nandi Stephen Sang  jumanne alishtakiwa kwa makosa matatu . Hakimu mkaazi  Beryl Omollo  aliyaaja mashtaka hayo kuwa uharibifu wa mali , uchochezi na kutumia vibaya maamlaka yake . Sang alikana mashtaka dhidi yake na mawakili wake kuitisha aachiliwe kwa dhamana .

Aliachiliwa huru kwa   bondi ya shilingi milioni Moja na mdhamini wa kiasi kama hicho au bondi ya shilingi elfu 500 pesa taslimu .

Kwa  uharibifu wa mali ,gavana huyo  anashtumiwa kwa kuharibu sehemu ya shamba la Chai la Kibware juni tarehe nane . mashtaka ya uchochezi yametokana na  matamshi yake kwa wafuasi wake kwamba wanafaa kujihami ili  kuwapokonya mashamba watu walionyakuwa ardhi za umma  likiwemo shamba la chai la Kibware .

Kwa kosa la kutumia vibaya maamla yake ,gavana huyo  anashtumiwa kwa kutumia trekta za serikali ya kaunti ya Nandi wakati wa uharibifu wa mimea cha chai . Alilala seli katika kituo cha polisi cha Central mjini Kisumu baada ya kukamatwa na maafisa wa DCI huko  Kapsabet.