Gavana Sonko alaumu ufisadi na kughushi kwa utendaji duni wa mapato jijini

sonko
sonko
Gavana wa Nairobi Mike Sonko amekiri kuwa rushwa na kughushi ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili katika ukusanyaji wa mapato katika kaunti hiyo.

Kulingana na Sonko, wakaazi wa jiji la Nairobi wamekuwa wahasiriwa wa utoaji wa leseni bandia na vibali vya biashara ambavyo vimewazuia kutolipa kodi kwa kaunti.

Imebainika kuwa tangu mwaka 2014, kaunti hiyo ya Nairobi haijawahi fikisha malengo yake.

 Mnamo Machi mwaka huu, ilifunuliwa kuwa kutokana na uimarishaji dhaifu, kaunti hiyo imekuwa ikipoteza mapato zaidi ya shilingi milioni 400,000 kutoka kwa masoko zaidi ya 43 humo jijini.

Ilionyeshwa zaidi kuwa malipo mengine bado yanafanywa kwa kaunti hiyo kutumia pesa ya mkononi licha ya Gavana Sonko kutangaza kuwa jiji hilo sasa linatumia mfumo ambao mtu hahitaji kuwa na pesa mkononi kwa minajili ya kulipia huduma mbalimbali.

Sonko alitaka tume ya maadili na kupambana na rushwa EACC kuungana naye kupigana na kesi za rushwa ambazo zimeathiri ukusanyaji wa mapato.

katika mwaka wa fedha 2017-2018 mapato yaliyokusanywa yalikuwa bilioni 10.25, dhidi ya lengo la bilioni 17.23