Gavana wa Kericho athibitisha kisa cha Ebola kimeripotiwa

Gavana wa Kericho Profesa Paul Chepkwony amethibitisha kisa kilichoripotiwa cha Ebola kaunti hiyo. Amewapongeza madakatari wa kaunti hiyo kwa kuchukua hatua za dharura katika kukabiliana na kisa hicho. Chepkwony amewahakikishia wakaazi kuwa kaunti hiyo iko tayari kukabiliana na ugonjwa huo. Wakati huo huo, matokea ya damu ya mgonjwa iliyotumwa jijini Nairobi ili kufanyiwa uchunguzi zaidi yanatarajiwa kutoka kabla ya mwisho wa siku. Afisa mkuu wa afya kaunti hiyo David Ekuwam anasema hali ya mgonjwa imeimarika kwa sasa.