king

Gavana Waiguru atishia kumshtaki King Kaka kuhusiana na wimbo “Wajinga nyinyi”

Gavana  wa Kirinyaga Ann Waiguru huenda akachukua hatua za kisheria dhidi ya msanii almaarufu King Kaka kuhusiana na ngoma yake “Wajinga nyinyi” ambayo imezua mdahalo mkubwa nchini.

Waiguru alidai wimbo huo ambao ulitolewa siku chache zilizopita, unaashiria kuwa gavana huyo ndiye mhusika mkuu wa kashfa ya NYS.

Katika barua ya Disemba 15, mawakili wa Waiguru Kiragu Watutha Advocates, wamesema kuwa msanii King Kaka alimtaja Waiguru kuhusika katika sakata mbalimbali za ubadhrifu wa raslimali za umma.

Mkewe rapa King Kaka afunguka kuhusu kibao cha ‘Wajinga Nyinyi’

 Waiguru aliongeza kuwa matamshi hayo hayana msingi wowote,  yamemchafulia jina  na kutoa dhana kuwa yeye ni tapeli.
.

King Kaka amepewa saa 48 kumuomba msamaha Waiguru na vile vile kutoa wimbo huo  “Wajinga nyinyi” kutoa mitandao yote ya kijamii.

Barua hiyo inasema kuwa King Kaka anapaswa kukubali makosa yake kupitia maandishi yasiyo na masharti na vile vile hapaswi kutoa nyimbo zozote zenye maneno mabaya dhidi ya mteja wao “Waiguru”

Aidha King Kaka alikumbushwa kuwa wimbo “Wajinga nyinyi” utakaposambazwa tena basi tukio hilo litasababisha hatua mpya ya dharua dhidi ya Waiguru.

William Ruto na Duale wananitishia maisha, Mutua aripoti kituo cha polisi

Mhariri: Davis Ojiambo.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments