Gavana Wilbur Otichilo Aapa Kuendelea Kufadhili Timu Ya Vihiga United

Wilbur Otichilo
Wilbur Otichilo

Gavana mteule wa kaunti ya Vihiga Wilbur Otichilo ametupilia mbali uvumi ambao umekua ukienezwa haswa kwa mitandao, ya kua serikali yake haitaunga mkono timu ya Vihiga United ambayo ni mmojawapo ya miradi ya maendeleo ambayo serikali ya aliyekua gavana wa kaunti hii Moses Akaranga ilianzisha.

Akizungumza katika uwanja wa Kidundu eneo bunge ya Vihiga, wakati aliyekuwa gavana Moses Akaranga alipokua akimkabidhi rasmi usimamizi wa timu hiyo  Gavana Wilbur Otichilo  amewahakikishia wachezaji hao kua hana nia yoyote ya kutowaunga mkono.