Gavana Wycliffe Oparanya aachana na azma yake ya urais

Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya ameachana na azma yake ya uaniaji kiti cha urais mnamo mwaka wa 2022 ili kumuunga mkono kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.

Akizungumza gavana huyo alisema kwamba angependa sana kupata uongozi wa chini na wala si gavana mwaka huo.

Pia alimwambia Raila kuwa endapo kuwa kiongozi amtafutia kiti huko wakati muhula na muda wake utakwisha.

"Naachia wengine siasa za kaunti baada ya muda wangu kukamilika, nataka kuagazia siasa za nchi na kumuuliza Raila kunitafutia kiti huko juu." Aliongea Oparanya.

Usemi wake unajiri siku chache baada ya gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua kuzindua zabuni yake ya urais, pia gavana wa kaunti ya Makueni Kivutha Kibwana alidai kuwa atawania kiti cha urais ifikapo mwaka wa 2022.

Je nani atakayeshinda katika kinyang'anyiro cha uwaniaji kiti cha urais, na je kinara wa ODM atawania kiti hivho?