Gay Husband! Mwanamke agundua mumewe ni mpenzi wa jinsia moja

sad woman
sad woman
Kuna vitu vingi ambavyo hufanyika katika ndoa vinavyosababisha fedheha na  na hisia za usaliti .

Kilichomfanyikia Redempta  kinazua machungu zaidi ya aina yoyote ya usaliti ambao mwanamke anaweza kupitia .Rede ,alikutana na  mume wake miaka mitano iliyopita baada ya kutambulishwa  kwake na rafikiye . baada ya muda sio mrefu walipendana na kuanza uhusiano ambao uliishia kuwa ndoa lakini mambo yalimbadilikia mwaka mmoja baada ya ndoa  yao alipoanza kugundua tabia ambazo sio za ‘mtu wa kiume’ katika mume wake .

‘ Alianza kujipodoa kupindukia na kujali sana kuhusu muonekano wake’  anasema.

 

 ‘Mwanzoni nilifiriki labda ni mazoea yake kwa sababu alikuwa msafi sana na hicho ni  mojawapo ya  vigezo vilivyonifanya  kumpenda,kila  vazi lak lilikuwa nadhifu na alikuwa na mpangilio maalum wa kila mambo yake’ anaongeza Redempta

Hata hivyo  Rede alianza kutialia shauku  mienendo ya mume wake alipoanza kujipaka rangi kwenye midomo yake kama mwanadada.Alianza hata kujitilia podari usoni alipokuwa akiondoka .Rafiki zake wa kiume pia walikuwa na tabia za kustaajabisha .Ingawaje sio ibaya kwa wanaume kukumbatiana ,Rede aligundua kwamba mumewe alikuwa na mazoea sana ya kufanya hivyo na  rafiki  zake wa kiume na alianza kupata hofu ya jinsi alivuokuwa akiangaliana na rafikiye wa karibu Andrew ambaye alikuwa akiwatembelea kila mara .

‘Angetumia saa kadhaa wakizungumza na Andrew,hata kuna wakati nilimuambia kwamba he spends more time with Andrew than me’ anasema Rede

Tabia  za mume wake na hsauku za watu zilianza kuwa nyingi na rafiki zake na hata jamaa zake wakaanza kumuuliza maswali kuhusu  mumewe .Wengi walikuwa wakimuuliza Rede iwapo mume wake alikuwa  ‘straight’ lakini aliyapuuza maswali kama hayo na kumtetea lakini katika moyo wake alikuwa na shauku zake.

Kilizuka kizaazaa siku moja wakati Redempta alipopata kanda ya video katika simu ya mumewe akiwa uchi na kupigana busu na mwanamme mwenzake! Alipoiangalia video hiyo hakuamini kwamba Yule alikuwa mumewe katika hali ile .Alishangaa lakini tena hakuwa na  sababu ya kutoamini alichoona kwa sababu kwa muda mrefu amekuwa akitafuta  ithibati ya kufahamu  ukweli kuhusu madai ambayo watu walikuwa wakitoa dhidi ya mume wake. Katika video nyingine kwenye simu hiyo Redempta aliweza kumuona rafiki wa mumewe Andrew pia akiwa uchi wa mnyama akifanya kisichoweza kuandikwa na wanaume wengine. Alihisi kusalitiwa na hakuwa na nguvu hata za kuweza kumkabili mumewe na ushahidi ule .Rede alishangaa mbona amekuwa amefumbwa macho kuweza kujua kilichokuwa kikifanyika puepe machoni pake . Aibu kwamba mumewe ni  mpenzi wa jinsia moja ni kitu ambacho kilimpa hofu ya kutoweza kuzungumza na wazazia wake na hata rafiki zake kuhusu yaliyompata . Alimuuliza mumewe kuhusu video zile na alichopata kama jibu kilimfanya kujiamulia kuondoka  ili aanze upya maisha yake .

Usaliti wa mwanamme aliyedai kumpenda na ugunduzi kwamba alikuwa ‘shoga’ ulimpa fikra nzito katika muda uliofuatia .Tangu wakati huo Redempta yungali katika lindi la mshtuko na kamwe  mazungumzo kuhusu uwezekano wake kuolewa tena yanamfanya kuchemka hisia na kutokwa machozi .