Geoffrey Majiwa aapishwa kama naibu spika wa bunge la Nairobi

Majiwa
Majiwa
Aliyekuwa meya wa  Nairobi na mwakilishi wa wadi ya Baba Dogo  Geoffrey Majiwa  amechaguliwa kuwa  naibu spika wa bunge la kaunti ya Nairiobi

Alithibitishwa  katika wadhifa huo na spika wa bunge hilo Benson Mutura  wakati wa kikao cha jumanne alasiri . Spika huyo aliutangaza kwamba hapakuwa na mgombeaji mwingine aliyekuwa amewasilisha stakabadhi zake kwa wakati ufaao .

Ni mwakilishi wa wadi ya Ngei  Redson Otieno  alikuwa ameonyesha nia ya kutaka kiti hicho lakini hakuwasilisha stakabadhi zake .

Kiti hicho kilisalia wazi baada ya JohnKamangu kujizulu alhamisi wiki iliyopita .