George Magoha atoa kauli, NBI yataja jumba la Precious Talent pango la kifo

unnamed__5___1569239661_36105
unnamed__5___1569239661_36105
Waziri wa Elimu George Magoha ameifunga shule ya msingi ya Precious Talent baada ya tukio la asubuhi.

Shule hii sasa itasalia kama imefungwa kwa muda wa siku 4 baada ya wanafunzi 7 na 64 kujeruhiwa.

"Shule hii inafungwa hadi Jumatatu baada ya ukaguzi wa jumba hili. Hatimaye tutatoa uamuzi mwafaka kuhusu hilo." Magoha

Soma hadithi nyingine:

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Magoha ametangaza kuwa wanafunzi 62 wamepata majeraha madogo madogo ila wawili wapo katika hali ya uangalizi wa kina.

Magoha aidha amewatetea maafisa wake wa kuhakiki ubora wa mijengo shuleni na kusema kuwa ubora wa mjengo huo uliteleza umakinifu wao.

Soma hadithi nyingine:

"Unaona kuwa mtu alijenga nyumba ya ghorofa juu ya nyingine...lazima nitetee afisa wangu wa kuhakiki ubora wa mijengo...kitu kama hiki kinaweza kukutoka na ukose kuona. Nitawajibika kuona kuwa kila kitu kipo sawa." Alisema Magoha

"Sijakuja hapa kulaumu mtu yeyote. Tukio moja la mjengo kama hili lisitumike kuwatia woga watoto wetu."

Soma hadithi nyingine:

Magoha amesema kuwa serikali itahakikisha usalama wa watoto bila kujali wanapotoka.

Katibu wa Mamlaka ya kutathmini ubora wa mijengo ametaja mjengo huo kama pango la kifo huku Moses Nyakiongora akisema kuwa tukio hilo ni kosa la uhalifu.